Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 December 2014
Thursday, December 25, 2014

Manchester United ni kiboko ya “Boxing day”


Na Chikoti Cico

Wakati timu za ligi kuu nchini Ujerumani (Bundesliga) na Hispania (la liga) zikiwa kwenye mapumziko katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka nchini Uingereza ligi hiyo itaendelea tarehe 26 “boxing day” kwenye viwanja mbalimbali katika mfululizo wa ratiba ngumu ya kipindi hiki cha sikukuuu.

Pamoja na kuwa ni kipindi ambacho timu zinacheza mechi nyingi katika muda mfupi kuna timu ambazo zinaonekana kuwa na takwimu nzuri katika kipindi hiki cha sikukuu katika kunyakua alama tatu muhimu.

Tukiangalia takwimu hizo timu ya Manchester United imeonekana kuwa ni kiboko katika kushinda mechi za “boxing day” katika ligi kuu nchini Uingereza, takwimu zinaonyesha katika mechi 22 walizocheza wamefungwa mchezo mmoja tu ambao ulikuwa ni dhidi ya Middlesbrough mwaka 2002 kwa kufungwa magoli 3-1.

Nayo timu ya Arsenal inashika nafasi ya pili katika timu zinaoongoza kushinda kipindi cha “boxing day” huku wakiwa wameshinda michezo 15, kutoka sare michezo sita na kufungwa mchezo mmoja kati ya michezo 22 waliyocheza.

Liverpool wanashika nafasi ya tatu ingawa hawajawahi kushinda siku ya “boxing day” toka mwaka 2010 alipoondoka kocha wao wa zamani Rafael Benitez.

Wakati huo huo timu zenye rekodi mbaya kwenye siku ya “boxing day” ni Swansea, Hull City na Burnley ambao hawajawahi kushinda mchezo wowote wa tarehe 26 Desemba huku wakiwa wamecheza michezo saba tu lakini katika timu zilizocheza mechi nyingi za boxing day na zenye rekodi mbaya zaidi ni Aston Villa ambo wameshinda michezo mitatu tu kati ya 22 na Everton ambao wameshinda michezo sita tu kati ya 22 ya boxing day.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!