Na Chikoti Cico
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal akataa kuzungumzia taarifa za timu hiyo kutoka jiji la Manchester kutaka kumsajili winga wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale.
Taarifa kutoka nchini Hispania zilizotoka Jumanne ya wiki hii zilisema Van Gaal yuko tayari kulipa ada ya kiasi cha pauni milioni 120 ili kumrejesha Bale kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza kuichezea United.
Akiongea na waandishi wa habari wiki hii kocha huyo kutoka nchini Uholanzi alipoulizwa kuhusu taarifa za kumsajili Bale alisema “ siwezi kujadiliana nanyi kuhusu hilo, ninajadiliana hilo na mtendaji mkuu wangu (CEO) na sio yeyote kwenye vyombo vya habari”
Hii sio mara ya kwanza kwa United kuonyesha kutaka kumsajili Gareth Bale kwani pia mwaka 2013 wakati anataka kuondoka Tottenham Hotspur.
United walitaka kumsajili lakini Real Madrid walishinda kwenye mbio hizo za usajili na kufanikiwa kupata saini ya Bale ambaye alisajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 86 akiweka rekodi mpya ya mchezaji ghali zaidi kusajiliwa.
Wakati huo huo utafiti uliofanywa siku ya Jumanne na gazeti moja la nchini Hispania kupitia mtandao wake wa AS.com wakiwauliza mashabiki wa Real Madrid kama watakuwa na furaha kama klabu yao itamruhusu Bale kuondoka kwa gharama sahihi.
Asilimia 54 ya mashabiki hao walikubali kwamba watakuwa tayari kumwachia mchezaji kuondoka Bernabeu.
0 comments:
Post a Comment