Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 December 2014
Wednesday, December 24, 2014

Kumbe Mourinho alimpa Ferguson mvinyo.


Na Chikoti Cico

Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho alitoa heshima zake kwa kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson wakati akihojiwa na Clare Blading kwenye mfululizo wa kipindi maalumu cha BT Sport kitakachorushwa siku ya tarehe 26 Desemba.

Katika mahojiano hayo pia Mourinho aliongelea utamaduni wa kunywa mvinyo pamoja na Ferguson kila baada ya mechi ambazo ziliwakutanisha makocha hao kwenye ligi kuu nchini Uingereza huku mara ya kwanza kabisa walipokutana kwenye uwanja wa Stamford Bridge mvinyo waliokunywa haukuwapendeza makocha hao.

Mourinho akielezea ilivyokuwa alisema “ilikuwa ni waandaaji wa chakula wa klabu ya Chelsea walionunua mvinyo na ni wazi mvinyo haukuwa na ubora ambao bosi (Ferguson) alistahili, ilikuwa inachekesha lakini inasikitisha.

Hivyo wakati ujao tulipocheza pamoja, nilimpigia rafiki na kumwambia nahitaji (mvinyo) bora na kuanzia hapo kila mara chupa ile ile wakati nikicheza dhidi ya bosi”

Katika kipindi hicho hicho maalum cha BT Sport Ferguson alihojiwa na kumzungumzia Mourinho huku akisema “si haki” kwa uwezo wa Mourinho kuzungumza lugha nyingi huku akiwa na mwonekano mzuri na kushinda vitu vyote.

Jose Mourinho alipoulizwa nini kimemfanya Ferguson awe maalum alisema “kila kitu, kipaji chake, muda alioweka kwenye kipaji chake katika huduma ya Manchester United na soka kwa ujumla.

Mapenzi yake aliyoweka kwenye kila kitu na baada ya hapo kwenye muda binafsi, wazi kabisa ni rafiki mzuri, mtu mzuri, hisia nzuri za ucheshi, nilimpenda sana”.

Aliendelea kusema “mara kwa mara nlikuwa na maswali ya kumuuliza na jinsi alivyoyajibu kwangu daima ilikuwa bora na msaada mkubwa”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!