Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 December 2014
Friday, December 26, 2014

Uchambuzi: Arsenal vs QPR


Na Chikoti Cico

Emirates Stadium nyumbani kwa timu ya Arsenal nyasi zitawaka moto pale ambapo wenyeji hao wataikaribisha timu ya QPR katika mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza katika siku ya Ijumaa yaani “Boxing day”.

Arsenal maarufu kama “washika bunduki wa London” baada ya kutoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Liverpool matokeo yaliyopelekea timu hiyo kushika nafasi ya saba wakiwa na alama 26 wanatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuingia “top four”.

Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger kuelekea mchezo huo atawakosa Laurent Koscielny, Aaron Ramsey, Mikel Arteta, Mesut Ozil, Abou Diaby, Jack Wilshere na Serge Gnabry ambao ni majeruhi.

Kwa upande mwingine,  kiungo Tomas Rosicky na kipa David Ospina ambao walikuwa majeruhi wakitarajiwa kuwepo kikosini kwenye mchezo huo dhidi ya QPR.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha timu ya Arsenal wana rekodi nzuri kwa mechi za “Boxing day” kwani katika michezo 17 iliyopita wameshinda michezo 11 huku wakifungwa mchezo mmoja na kutoka sare michezo mitano.

Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Szczesny, Chambers, Debuchy, Mertesacker, Monreal, Flamini, Rosicky, Walcott, Sanchez, Giroud, Welbeck.

Kwa upande wa QPR matokeo ya mechi iliyopita dhidi ya West Brom ambapo walishinda kwa magoli 3-2 hivyo kupelekea kushika nafasi ya 16 wakiwa na alama 17 yameiongezea nguvu na ari timu hiyo hivyo wataingia kwenye mchezo dhidi ya Arsenal kutafuta ushindi kwa nguvu zote ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuondoka kwenye hatari ya kushuka daraja.

Kocha wa QPR Harry Redknapp kuelekea mchezo huo atawakosa beki wa kushoto Yun Suk-Young ambaye ni majeruhi pia ataendelea kuwakosa Sandro na Alejandro Faurlin ambao pia majeruhi lakini pia kocha huyo ameweka wazi kwamba ana wachezaji wengi ambao wameumia na watachunguzwa kuelekea mchezo huo.

Kuelekea mchezo huo takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa QPR Charlie Austin anaongoza kwa magoli kati ya washambuliaji wa Kiingereza kwenye msimu huu wa ligi huku akiwa amefunga jumla ya magoli 11 mpaka sasa.

Kikosi cha QPR kinaweza kuwa hivi: Green, Onuoha, Dunne, Caulker, Yun, Hoilett, Barton, Kranjcar, Mutch, Fer, Austin

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!