Timu saba zamgombea Hamis Kiiza.
Na Oscar Oscar Jr
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mganda Hamis Kiiza ambaye ameachwa na klabu ya Yanga katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni kwenye ligi kuu Tanzania bara, amewasili nchini leo kwa lengo la kupata barua rasmi na taratibu nyingine ambazo zimehusishwa kutemwa kwake na klabu hiyo.
Akizungumza na kituo cha Redio cha E-FM kwa njia ya simu, mchezaji huyo ambaye msimu uliopita aliweza kufunga mabao zaidi ya 10, amesema kuwa tayari ana ofa kama saba hivi kutoka nchi saba tofauti ambazo zinamuhitaji.
Alipoulizwa kama klabu ya Simba ilimuhitaji katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibu, Kiiza alikiri kuwepo na ofa kutoka Simba lakini muafaka haukufikiwa.
Mshambuliaji huyo wa Uganda amekiri kuwa ndani ya siku nne hadi saba tayari atakuwa amesaini mkataba na klabu ya nje ya nchi na kila mtu ataifahamu timu hiyo ambayo amegoma kuiweza wazi.
Alipotafutwa Clement Sanga kuzungumzia swala la mchezaji huyo, alikiri kuwa hakuna tatizo na taratibu zote zitafanyika kama ilivyokuwa kwa watendaji wengine wa benchi la ufundi ambao mikataba yao ilikatishwa kwa hiyo hakuna tatizo lolote.
0 comments:
Post a Comment