Na Chikoti Cico
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho ageuka mbogo na kumshutumu mwamuzi aliyechezesha mechi kati ya Southampton dhidi ya Chelsea mchezo uliochezwa jana na kuisha kwa sare ya goli 1-1.
Mwamuzi wa mchezo huo Anthony Taylor ambaye alimpa kadi ya njano Cesc Fabregas kwa kuonekana kama alijiangusha kwenye eneo la penati la Southampton lakini marudio ya video yalionyesha Fabregas aliangushwa na beki wa timu hiyo tukio lililoamsha hasira ya Mourinho dhidi ya mwamuzi.
Akiongea baada ya mchezo huo Mourinho huku akionekana kugadhabika kwa tukio hilo alisema “Waamuzi hawako hapa kubuni, wako hapa kuona, alidhani Cesc hakuwa mwaminifu na alikosea, mechi baada ya mechi makocha wanasema wachezaji wa Chelsea wanajiangusha, bila kutatarajia Sam Allardyce aliongelea kuhusu wachezaji wangu”
“Nitaenda kwa mwamuzi, kumtakia mwaka mzuri na kumweleza aone aibu, kuna kampeni dhidi ya Chelsea, kwenye Nchi nyingine ambazo nimefanya kazi kabla, kesho kwenye magazeti ya michezo ingekuwa ni skendo ukurasa wa mbele kwasababu ni skendo”.
“Katika nchi hii ninafuraha na hilo tena zaidi ya furaha tutasema lilikuwa ni kosa kubwa lenye ushawishi mkubwa kwenye matokeo. Ninafuraha kwamba ndiyo jinsi lilivyo nikiwa na heshima kwa mwamuzi, alifanya kosa kubwa kama ninayofanya, kama wachezaji wanavyofanya”.
0 comments:
Post a Comment