Katibu mkuu wa Yanga afikishwa Polis
Na Oscar Oscar Jr
Klabu ya Yanga kupitia kwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga wamethibitisha kushiriki michuano ya Mapinduzi ambayo itafanyika mapema mwezi Januari huku wakiwahakikishia wapenzi wa soka visiwani Zanzibar kuwa watapeleka kikosi kamili.
Akizungumza na kituo cha Redio cha E-FM, Sanga amesema kuwa Yanga wamejipanga kwa michuano hiyo na watapeleka kikosi chao cha kwanza kuhakikisha wanatoa ushindani na kudumisha mahusiano mazuri na wadau wa soka visiwani humo.
Yanga ambao wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na alama 14, watalazimika kukatisha mechi zao za ligi kuu ambapo mchezo wao unaofuata walitakiwa kusafiri kuelekea Jijini Mbeya kuwakabili vijana wa kocha Juma Mwambusi, timu ya Mbeya City.
Kwa upande mwingine, aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo bwana Benno Njovu ameweza kuvunja ukimwa na kueleza kadhia iliyoko mbele yake ambapo anadaiwa kufuja fedha za klabu hiyo wakati akiwa madarakani.
Akizungumza na mtangazaji wa E-FM, katibu huyo ameonyesha kusikitishwa na habari hizo ambazo amekiri na yeye kuweza kuzisikia na tayari amekwenda Polis kutoa maelezo huku uchunguzi ukiendelea kufanyika.
Kuhusu kutimuliwa na klabu hiyo, Njovu amesema hakutimiliwa isipokuwa mkataba wake ulimalizika na alipoulizwa namna anavyoweza kumtabiria katibu mkuu mpya wa timu hiyo, Njovu amesema haweza kumtabiria chochote.
Pamoja na katibu hiyo kutosema chochote, ameonyesha kusita kuashirikia kuwa mambo ni magumu kufanya kazi kwenye nafasi hiyo hasa katika Uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti Yusuph Manji.
0 comments:
Post a Comment