Simon Msuva hatakiwi kujisikia mnyonge.
Na Samuel Samuel
Kuna uwezekano mkubwa sana kwa mdogo wangu, Saimoni Msuva kuja kupotea ghafla kwenye vichwa vya habari za soka hapa nchini.
Kiasilia Msuva ni kiungo mchezeshaji na akiwa mkoani Moro alikuwa akicheza kiungo cha juu na wakati mwingine, anafanya vizuri kama atatumika kama kiungo mshambuliaji.
Kuna muda Yanga walimtumia katika nafasi hiyo na aliitendea haki lakini kitaalamu Msuva sio aina ya mchezaji mwenye uwezo wa kucheza @one - two passes" na hivyo nafasi ya kushambulia akitokea pembeni ndiyo inaonekana kumfaa zaidi.
Msuva ndiye mfungaji bora mpaka sasa kwa upande wa timu ya Yanga akiwa na mabao matatu na tayari akili yake ina amini kuwa akitoka uwanjani bila kufunga, anakuwa hajatimiza wajibu wake. Hili ni tatizo.
Akili ya Msuva inatakiwa kuwaza zaidi kuichezesha timu na kutengeneza kutengeneza nafasi za kufunga kuliko kufunga kwenyewe. Kama anapata nafasi ya kufunga sio jambo baya lakini asijisikie unyonge pale anapotoka uwanjani bila kufunga.
Toka aisawazishie Yanga mechi na Simba na matokeo kusomeka 1-1, amekuwa akiua sometimes move za goli kwa washambuliaji hasa kwa kutaka kufunga yeye mwenyewe.
Lazima ajengwe kisaikolojia hata kwa ili aweze kuamini kuwa, hata pasi za mwisho bado zinaweza kumfanya aonekane bora na sio lazima afunge.
Ukitazama mechi ambazo Msuva anatoka uwanjani bila kufunga huwa anakuwa mnyonge sana na hata mashabiki humuona yupo nje kimchezo.
Hali hii inaweza kuja kumfanya mchezaji huyo akapotea ghafla wakati anaonekana bado hajafika hata kwenye kilele cha ubora wake.
0 comments:
Post a Comment