Searching...
Image and video hosting by TinyPic
22 December 2014
Monday, December 22, 2014

Mourinho adai leo ni fulu mziki!

Na Oscar Oscar Jr

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amezungumza kuelekea mpambano wake wa leo ugenini kwenye dimba la Britania ambapo anakwenda kukutana na timu ya Stoke City ambayo inakamata  nafasi ya 13 wakiwa na pointi 19 kwenye msimamo wa ligi kuu.

Mourinho ameulizwa kama anaweza kuwapa nafasi wachezaji kama  Petr Cech, Filipe Luís na Mikel John Obi ambao hivi karibuni wameonyesha viwango vya juu.

Akijibu swali hilo, Mourinho ameonyesha wazi kuwa wachezaji kama Thibaut Courtois , César Azpilicueta  na Cesc Fàbregas wote wanatarajia kurejea kwenye kikosi cha kwanza na hakuna uwezekano wa Mikel Obi, Cech na Luiz kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.

Mourinho ameongeza kuwa hakuna mchezaji anayejisikia vibaya kwa kitendo cha kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwani wao kama timu, lengo lao ni kuhakikisha timu inashinda bila kujali nani ameanza dimbani na yupi ameanzia benchi.

Chelsea watakuwa wageni wa Stoke City kwenye mchezo wa 17 wa ligi kuu Uingereza ambao unatarajiwa kuchezwa majira ya saa tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Endapo Chelsea wataibuka na ushindi, wataongeza mwanya wa tofauti ya alama tatu kati ya yao na Manchester City ambao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 39 ambazo ni sawa na walizonazo Chelsea.

0 comments:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!
Enjoy this page? Like us on Facebook!)