Rais wa Simba ampa tano Aden Rage.
Na Oscar Oscar Jr
Hata kama mtu amekuwa mbaya kiasi gani, kuna muda anapofanya jambo la maendeleo inabidi kupongezwa. Hivyo ndivyo unavyoweza kutafsiri kauli ya Rais wa Simba, Evance Aveva akimzungumzia aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Mh. Ismail Aden Rage.
Rage ni moja kati ya viongozi wa Simba waliomaliza utawala wao huku wakiwa na lawama nyingi sana kwa wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kongwe. Moja kati ya mambo yaliyofanya Rage kulaumiwa ni kuuza baadhi ya wachezaji nyota wa timu hiyo bila kujulikana pesa zilikokwenda.
Wapo waliodai kiongozi huyo alitafuna fedha hizo, wapo pia waliodai kuwa alikuwa anaitumia klabu hiyo kwa manufaa yake binafsi.
Moja kati ya wachezaji waliouzwa chini ya Rage ni mganda, Emmmanuel Okwi kwenda klabu ya Etoile du Sahel ya nchiniTunisia na uhamisho huo uliiibua maswali mengi kuliko majibu.
Baada ya kushutumiwa kuwa Mwenyekiti huyo alipokea pesa, hivi karibuni kupitia kwa Rais wa sasa wa Simba, ukweli umebainika kuwa Rage hakula pesa yoyote na Simba wameshinda rufaa yao ambaye walikata kwenye shirikisho la soka duniani (FIFA).
Aveva hakusita kumpongeza na kumsifia Mwenyekiti Aden Rage kwa namna alivyopambana kuhakikisha timu inapata haki yake. Aveva amesema Rage alikuwa sambamba na Uongozi wake kuhakiksha kuwa Simba inanufaika na uhamisho wa mchezaji huyo ambaye kwa sasa, amerejea tena kuitumikia klabu hiyo na anaonekana kurejea kwenye ubora wake.
Klabu ya Etoile Du Sahel imepewa siku 30 kuhakikisha kuwa, wanalipa dola 300,000 kwa klabu ya Simba ambazo ni zaidi ya Milioni 500 kwa pesa za kitanzania. Aveva amesema zile ni fedha za klabu na sio za mchezaji kwa hiyo ni Simba ndiyo watakaonufaika na pesa hiyo.
0 comments:
Post a Comment