Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Balotelli hakamatiki!!


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya Liverpool ya Uingereza, Mario Balotelli amepatikana na hatia ya kuvunja sheria ya matumizi ya mitandao ya jamii ya chama cha soka cha Uingereza (FA). kitendo kilichopelekea mchezaji kufungiwa kwa mechi moja na kupigwa faini ya kiasi cha pauni 25,000.

Balotelli alipatikana na hatia hiyo baada ya kuweka picha kwenye mtandao wa Instagram mapema mwanzoni wa mwezi Desemba na baada ya uchunguzi wa chama cha soka cha Uingereza picha hiyo ilionekana kuwa ni tusi ama fedheha na hivyo Balotelli kupatikana na hatia.

Pamoja na kutumikia adhabu ya kutokucheza mchezo mmoja wa ligi kuu nchini Uingereza ambao utakuwa ni kati ya Liverpool dhidi ya Arsenal hapo Jumapili na kulipa faini pia Balotelli atatakiwa kuhudhuria kozi maalum ya elimu ya matumizi ya mazuri ya mitandao ya jamii.

Baada ya uamuzi huo wa FA kutolewa Balotelli aliomba msamaha kwenye ukurasa wake wa tweeter kwa kuandika kuwa “kufuatia tukio linalohusiana na bandiko langu la Super Mario, uamuzi wa FA umeweka wazi kwamba ni kosa.

Samahani kwa wachezaji wenzangu na mashabiki wa Liverpool wameadhibiwa kwa kitu nilichokifanya na sasa nimekuja kujutia. Ni dhamira yangu kukubaliana na uamuzi wa FA na kuhakikisha kwamba hakitatokea tena”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!