Bayern Munich wazidi kutamba Bundesliga.
Na Oscar Oscar Jr
Frank Ribery ambaye msimu uliopita alishika nafasi ya tatu kwenye tuzo za mchezaji bora wa mwaka wa Dunia maarufu kama Ballon D'or, nyuma ya Lionel Messi na Christiano Ronaldo, jana aliweza kufunga bao pekee lililowapa ushindi timu ya Bayern Munich wa bao 1-0 mbele ya Bayern Leverkusen.
Ushindi huo umeongeza mwanya wa alama saba kwenye Bundesliga kati ya vinara Bayern Munich dhidi ya timu ya Wolfsburg ambao wanakamata nafasi ya pili mara baaada ya kupata ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Hannover.
Kiungo wa zamani wa Chelsea, Kevin De Bruyne alifungua mvua ya magoli ya Hannover kwenye mchezo huo wa siku ya Jumamosi huku Bayern Leverkusen wakishuka hadi nafasi ya tano.
Huu ulikuwa mchezo wa 287 kwa Ribery akiwa na Bayern. Ushindi huo ni dalili njema za kuendeleza mbio za kocha Pep Gaurdiola kutaka kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita.
Borussia Dortmund ambao msimu uliopita walimaliza kwenye nafasi ya pili, weekend hii wameweza kuchomoka mkiani baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Hoffenheim.
0 comments:
Post a Comment