Polis Morogoro wameleta Mpya!
Na Oscar Oscar Jr
Mara nyingi sana timu za Majeshi zimekuwa na utamaduni wa kuongozwa na viongozi ambao ni wanajeshi wenzao. Timu kama Rinho Rangers ya Tabora, Polis Dar es saam, Tanzania Prisons ya Mbeya na JKT Oljoro ni moja ya mifano hai ambayo inaonyesha ni kwa namna gani Majeshi yamekuwa na utamaduni huo ambao Polis ya Morogoro imeamua kukiuka na kutoa nafasi kwa raia.
Timu za majeshi zimekuwa hazifanyi vuizuri sana na moja ya sababu inatajwa kuwa na viongozi ambao hawana uwezo wa kuongoza soka na badala yake wamekuwa wakipewa nafasi kwa kigezo tu cha kuwa wanajeshi.
Polis Morogoro imefanya uchaguzi mkuu juzi mkoani Morogoro na kujipatia viongozi wake ambao wanamchanganyiko wa Wanajeshi na Raia. Timu hiyo pia imepanga kutoa kadi kwa ajili ya mashabiki na kutoa fursa kwa wakazi wa morogoro kuwa sehemu ya timu hiyo.
Polis Morogoro ambayo inakamata nafasi ya nane ikiwa na pointi tisa kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, kwa sasa itaongozwa na Mwenyekiti Zuberi Chembera na makamu wake Odira Tweve ambao wote ni raia.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi za majeshi kwa siku za hivi karibuni kuongozwa na viongozi wa juu ambao sio wanajeshi. Polis Morogoro watashuka dimbani Desemba 28 kwenye dimba la Jamhuri Morogoro kuwaalika Mgambo shooting ya mkoani Tanga.
0 comments:
Post a Comment