Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 December 2014
Wednesday, December 24, 2014

Azam waitunishia misuli El-Merreikh ya Sudani.


Na Oscar Oscar Jr

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Azam kupitia kwa mtendaji mkuu wa timu hiyo, bwana Sad Kawemba,  wameleza namna ambavyo wamejipanga kuhakikisha wanatetea ubingwa wao msimu huu.

Akizungumza na kituo cha Redio one  asubuhi ya leo, Mtendaji huyo pamoja na mambo mengine, amezungumza nia ya Azam ya kuhakikisha wanakuwa vinara wa ligi kuu kabla ya kuanza kushiriki michuano ya klabu bingwa  Afrika ambayo wamepangwa na mabingwa wa Sudan, timu ya El-Merreikh.

Azam ambao wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu  Tanzania bara wakiwa na alama 13, tarehe 28 Desemba watashuka uwanjani kucheza na timu ya Yanga ambao wanakamata nafasi ya pili licha ya timu hizo kuwa na alama sawa na ili Azam wawezaa kurejea kileleni ni lazima waanze na ushindi kwenye mchezo huo.

Pia bwana Kawemba hakusita kuzungumzia mahusiano mazuri yanayoendelea kati yao na klabu ya El Merreikh ambayo yalipelekea Azam kuweza kumnasa beki wa kati ambaye ni raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa ambaye alikuwa na mabingwa hao wa Sudan kwa muda mrefu.

Pamoja ya hayo, Kawemba hukusita pia kuonyesha namna Azam inavyowaheshimu Wasudani hao lakini alibainisha kuwa hawaiogopi timu hiyo na ana matumaini makubwa ya kuwaondoa wababe hao wa Sudan watakapokutana na Azam kuweza kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!