Searching...
Image and video hosting by TinyPic
20 December 2014
Saturday, December 20, 2014

Kijana wa Liverpool ashinda tuzo barani Ulaya.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa Liverpool, Raheem Sterling ameshinda tuzo ya mchezaji bora kijana barani Ulaya kwa mwaka 2014 (2014 European Golden Boy).

Sterling ameshinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia Liverpool kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kwa mwaka 2013/2014 pia aliiwezesha timu ya taifa ya Uingereza kucheza kombe la Dunia huku pia akishiriki kucheza kwenye michuano ya kufuzu kombe la Ulaya kwa mwaka 2016.

Mchezaji huyo mwenye miaka 20 amenyakua tuzo hiyo baada ya kuwapita wachezaji wengine 40 kutoka ligi mbalimbali duniani zikiwemo La liga, Bundesliga, Serie A na League 1, tuzo hiyo hutolewa kwa mchezaji aliye chini ya miaka 21 na anayecheza kwenye ligi kubwa barani Ulaya.

Baada ya kupokea tuzo hiyo akiongea na mtandao wa Liverpool Sterling alisema “Ni mafanikio makubwa kushinda tuzo ya namna hiyo, ni hisia ya furaha hakika kwangu na familia yangu, kitu ambacho mara zote nilitaka kufanya ni kucheza kwa bidii na kujaribu kutambulika, nashukuru sana kwamba watu wameonyesha kunitambua”

“Ni kwaajili ya bidii, ninafuraha sana kwamba watu wametambua kwamba ninajaribu kufanya kazi kwa bidii na kufanya vizuri kwaajili ya klabu hii, hakika ninashukuru kwa tuzo hii”

Nao timu ya Liverpool walimpongeza mchezaji wao huyo kwa kuandika kwenye ukurasa wao wa tweeter ujumbe unaosomeka kwamba “Hongera Sterling 31 ambaye leo ametangazwa kama mshindi wa tuzo ya heshima ya mchezaji bora kijana Ulaya kwa mwaka 2014”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!