Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 January 2015
Friday, January 09, 2015

Podolski amsemea mbovu Wenger.


Na Chikoti Cico

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Lucas Podolski ambaye kwasasa anaichezea kwa mkopo timu ya Inter Milan akitokea Arsenal akerwa na jinsi ambavyo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alivyomwacha aondoke bila ya kumuuaga.

Podolski ambaye kwa muda mrefu alikuwa akikaa benchi wakati akiichezea Arsenal kabla ya kulazimisha kuondoka kwenye kabla hiyo yenye makazi yake jijini London akiongea na vyombo vya habari alisema:

“hakusema chochote kwangu, hakunipigia simu ama kusema kwaheri, sihitaji maua ama busu kutoka kwake lakini ni kuhusu heshima, kuhusu kusema kwaheri. Kwangu heshima ni muhimu”.

Aliendelea kusema “nilifanya kila kitu ambacho ningeweza kwaajili ya klabu, siamini nilifanya chochote kibaya, sikulewa klabuni”.

Pia Podolski aliwashukuru mashabiki wa Arsenal na kuzungumzia usajili huo wa kwenda Inter Milan kwa kusema “nilikuwa na muda mzuri Arsenal, nataka kuwashukuru mashabiki na klabu, sikucheza sana na Inter walinipa nafasi.

Nilikuwa na mazungumzo mazuri na (Roberto) Mancini na alinifanya iwe rahisi kuja. Ninakuwa bora nikicheza katikati kama namba 10 au kama mshambuliaji lakini tutaona nini meneja anataka”.

Wakati huo huo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa kwamba hakumuaga Podolski kwa kusema “nikataa hilo kabisa, nilikuwa na mazungumzo nae kuhusu kwenda kwa mkopo, alihitaji ruhusa yangu na nilimpa nafasi yangu”.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!