Searching...
Image and video hosting by TinyPic
9 December 2014
Tuesday, December 09, 2014

HENRY JOSEPH KAWASAHIHISHE WIKIPEDIA





Na Chikoti Cico


Unaujua mtandao wa WIKIPEDIA? Inawezekana likawa ni swali gumu kwa Watanzania wengi ambao taarifa zao nyingi wanazipata kupitia magazeti ya kila siku yanayochapishwa nchini. Lakini kwa wale watumiaji wa “Internet” katika kutafuta taarifa wataweza kuwa wanaufahamu mtandao huu.

WIKIPEDIA ni mtandao ulioanza kufanya kazi mwaka 2001 na unamilikiwa na shirika la WIKIMEDIA FOUNDATION kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali na kwa lugha tofauti tofauti huku wasomaji wakiwa na uwezo wa kuhariri kurasa mbalimbali zilizowekwa kwenye mtandao huo.

Baada ya kueleza kwa ufupi kuhusu WIKIPEDIA hebu tuingie kwenye makala yetu yenye kichwa “Henry Joseph kawasahihishe Wikipedia”, ndiyo ukiingia kwenye kurasa inayumzungumzia kiungo huyu mahiri wa zamani wa Simba utakutana na makosa ambayo ni muhimu kusahihishwa.

Mwanzo kabisa mwa ukurasa unaomzungumzia Henry Joseph baada ya kuelezea kwamba amezaliwa Mwanza Tanzania, Tarehe 3 November 1985 kuna maneno yakaongezwa “He currently plays for Kongsvinger” wakimaanisha kwasasa anaichezea timu ya Kongsvinger ya nchini Norway.

Na kwenye maneno hayo ndipo ambapo Henry Joseph anajhitajika kutembelea mtandao huo na kuhariri kwamba “he currently plays for Mtibwa Sugar” kwamba kwasasa anaichezea Mtibwa Sugar, baada ya mchezaji huo karibuni kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo kutoka Morogoro kwaajili ya kuichezea kwenye ligi kuu nchini Tanzania.

Lakini mantiki nzima ya makala haya sio Henry Joseph kwenda kuhariri ukurasa wake kwenye mtandao wa WIKIPEDIA bali ni jinsi gani kuna faida kubwa kuzichezea timu za nje ambapo hata taarifa zako ni rahisi kuwekwa kwenye mitandao mbalimbali ya habari na taarifa hizo kukusaidia kupiga hatua kisoka.

Akiwa na umri wa miaka 29 tayari Henry anaonekana amechoka wakati hiki ni kipindi ambacho angetakiwa kuwa ameingia mkataba mwingine na timu kubwa zaidi ya Kongsvinger lakini hapana kilichotokea ni mkataba wake kuisha na akaamua kurejea nyumbani kuichezea Simba na sasa Mtibwa Sugar.

Hatuwezi kukataa kwamba mambo yakienda kombo ughaibuni ni vizuri kurejea nyumbani lakini kwa hili la Henry ni ngumu kumwelewa kwanini alikubali mkataba wake kuisha bila kuongezewa mkataba mwingine tena wenye maslahi zaidi?

Unaweza ukaona ni kitu cha kawaida sana ila kwa mkataba wa mchezaji kuisha bila kuongezewa mwingine inawezekana sababu zikawa ni kiwango kushuka hii ikiwa sababu kubwa zaidi, utovu wa nidhamu ama majeraha ya mara kwa mara hivyo kwa tunaomjua Henry sababu ya kwanza inaonekana wazi kuwa chanzo cha yeye kutokupewa mkataba mpya na Kongsvinger.

Sasa unawaza kwa mtoto wa kitanzania ambaye anataka kucheza soka Ulaya ataiga kwa nani? atajifunza kwa nani? ama ataomba ushauri kwa nani? hapa ndipo ambapo ntabaki kumlalamikia Henry Joseph kwa kuwa mrahisi kuacha nafasi yake nchini Norway kuchukuliwa na mchezaji mwingine.

Na katika hili tutabaki kuwasifia kina Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kwa kuendelea kudumu kwenye timu ya TP Mazembe ya nchini Kongo lakini ukweli utabaki kuwa Kongo haiwezi kuwa “Ulaya yetu”.

Ila kama mpaka leo mtandao wa WIKIPEDIA unasema kwamba Henry anakipiga Kongsvinger badala ya Mtibwa Sugar basi inawezekana huko ndipo alistahili kuwepo.
NAWASILISHA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!