Na Samuel Samuel 0652-464525
July mwaka huu dunia nzima ya wapenda soka ilishituka pale miamba ya soka duniani Brazil walipokuwa wanapokea kichapo cha mbwa mwizi toka kwa Ujerumani. Mechi hiyo ya nusu fainali kombe la dunia imebaki kuwa kumbukumbu mbaya kabisa katika taifa hilo la wapenda soka. Ujerumani iliwafunga Brazil goli 7-1.
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo wadau wa soka , wachambuzi mahiri wa soka na baadhi ya wachezaji mahiri waliwahi kutamba na kikosi hicho , waliubeza uteuzi wa timu hiyo iliyokuwa na wakali kama Neymar, William na Osca.Kocha Luis Fellipe Scolari alikomaa na kukiamini kikosi chake lakini mwisho wa siku ni kulitia aibu taifa hilo
Viongozi wa Simba SC hawana tofauti kubwa na Fellipe Scolari , tofauti kubwa wao ni watawala na Fellipe alikuwa mwalimu wa soka. Wakati mcroatia Loga anarudi kusaini mkataba mpya alishangazwa sana na usajili uliofanywa na viongozi hao.
Wengi wa wachezaji walikuwa ni wakaida sana wanaokosa kitu cha ziada kama wapiganaji sahihi wa kutafuta kombe la ligi kuu ( average players and not complete players). Loga alifikia kusema " sitaki wachezaji hawa na nileteeni watu wa kazi) Loga alijikuta akipigwa mkwara na kunyamaza kimya.
Lakini Mungu alimwinamia Loga na kauli yake baada ya Simba SC kupokea kichapo siku ya Simba day toka kwa Zesco. Timu hiyo toka Zambia iliibamiza Simba SC goli 3 .
Sikio la kufa halisikii dawa . Viongozi badala ya kuikumbuka kauli ya Loga wao wakaamua kumfukuza kabisa. Walimfukuza kocha huyo lakini hata ligi ilipoanza zimwi la Loga liliendelea kuwatafuna baada ya kutoka sare michezo sita na kushinda mchezo mmoja tu kwa mbinde dhidi ya Ruvu Shooting (1-0).
Ifike wakati viongozi wa soka nchini watambue kazi za makocha na kuziheshimu. Ligi imesimama na bado kauli ya Loga inapumua vifuani mwa viongozi wa Simba hata kama hawataki kukiri. Express ya nchini Uganda imetoka droo na Simba kabla ya kufungwa na Yanga .
Tukio baya zaidi ni juzi baada ya Mtibwa Sugar kuibamiza klabu hiyo kongwe goli 4-2. Usajili wa klabu hiyo chini ya Hans Pope umeshindwa kuijenga klabu hiyo kiufundi na kugeuka washindani halisi.
Tazama usajili wa Kiongera, Okwi na jinsi alivyo achwa Donald Musoti ni miujiza tu . Kipigo cha goli nne toka kwa Mtibwa nadhani kitawakumbusha kauli za Loga. Simba inajiandaa kuivaa Yanga tarehe 13 Dec tusubiri tuone kama kutakuwa na mabadiliko yoyote yale.

0 comments:
Post a Comment