Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 December 2014
Saturday, December 27, 2014

Fellaini nje mpaka mwakani.


Na Chikoti Cico

Kiungo wa timu ya Manchester United, Maroune Fellaini anatarajiwa kukosa michezo yote ya Krismasi na mwaka mpya baada ya kugundulika kwamba ana majeraha ya mbavu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Kocha wa Manchester United mdachi Luis va Gaal mapema Ijumaa kabla ya mchezo dhidi ya Newcastle alitoa taarifa mbele ya vyombo vya habari kwamba mchezaji huyo atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na virusi visivyoeleweka lakini baada ya mchezo huo taarifa zilisema Fellaini atakosekana kwenye mchezo dhidi ya Spurs hapo Jumapili kutokana na majeraha ya mbavu.

Kiungo huyo mkabaji kutoka Ubegiji aliyesajiliwa na United kutoka Everton aliumia mbavu kwenye mchezo wa Desemba 14 dhidi ya Liverpool na kutokana na kuumia huko Fellaini anatarajiwa kurejea uwanjani bada ya mchezo wa raundi ya tatu wa kombe la FA dhidi ya Yeovil.

Wakati huo huo taarifa njema kwa kocha wa Manchester United Louis Van Gaal ni kwamba wachezaji wengine ambao walikuwa majeruhi kama Daley Blind, Marcos Rojo na Luke Shaw wanakaribia kurejea uwanjani baada ya kukosakana kwenye mechi zilizopita.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!