Searching...
Image and video hosting by TinyPic
27 November 2014
Thursday, November 27, 2014

Varmelen nje miezi mitano.


Na Chikoti Cico

Taarifa kutoka timu ya Barcelona zinasema Thomas Varmelen anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa paja na mtaalam wa upasuaji kutoka nchini Finland aitwae Sakari Orava ili kuweza kumnusuru mchezaji huyo na kushindwa kucheza kabisa kwasababu ya kuumia huko.

Mtaalam huyo wa upasuaji anasifika kwa kumtibu mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Jonathan Woodgate ambaye majeraha yake yalimfanya asicheze kwa msimu mzima kwenye msimu wa mwaka 2004 pia daktari huyo aliwahi kuwafanyia upasuaji David Beckham na Pep Guadiola kipindi cha nyuma.

Beki huyo aliyesajiliwa toka timu ya Arsenal atakuwa nje kwa muda wa miezi minne mpaka mitano baada ya kufanyiwa upasuaji huo kabla ya kurejea tena uwanjani mwanzoni mwa mwaka 2015.

Varmelen alipata majeraha hayo wakati akiichezea timu yake ya taifa ya Ubelgiji dhidi ya Russia miezi mitano iliyopita kwenye michuano ya kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazili.

Mpaka sasa beki huyo anayetumia mguu wa kushoto hajaichezea Barcelona mchezo wowote wa mashindano huku akiwa amecheza kwa dakika 72 tu katika moja ya michezo ya kirafiki ya timu hiyo kutoka Catalunya.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!