Na Chikoti Cico.
Timu ya Real Madrid ya nchini Hispania imebadili nembo yake inayoonekana kwenye jezi baada ya kuingia mkataba mpya na National Bank of Abu Dhabi, timu hiyo imeondoa msalaba mdogo wa kikristo unaoonekana juu ya nembo hiyo maalum kwa timu ya Madrid.
Real Madrid ambao wanaongoza ligi kuu nchini Hispania maarufu kama la liga wakiwa na alama 33 baada ya kucheza michezo 13 wamefikia uamuzi wa kuondoa msalaba huo mdogo kwenye nembo yao ili kutoa fursa kwa mashabiki wa kiislamu kutoka falme za kiarabu (UAE) ambako ndipo wadhamini hao wanatoka.
Raisi wa Real Madrid Florentino Perez aliungana na kina Gareth Bale, Karim Benzema, Dani Carvajal na Toni Kroos wakati wa kutangaza udhamini huo mpya wa National Bank of Abu Dhabi mapema wiki hii.
Akiongea kwenye hafla hiyo Perez alisema “ Najua kwamba watu wanapata uzoefu kwenye kila mechi kwa namna ya pekee na kwamba muunganiko wetu na UAE unaendelea kukua zaidi, makubaliano haya yatasaidia kuendelea kukonga nyoyo za mashabiki katika Falme za kiarabu”
0 comments:
Post a Comment