Na Oscar Oscar Jr
Na Oscar Oscar Jr
HATIMAYE timu ya Simba imeweza kuvunja mwiko wa kutopata ushindi kwenye michezo yake yote ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Simba jioni ya leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting na kufikisha pointi tisa kutokana na kushuka dimbani mara saba huku bao hili likifungwa na Mganda, Emmanuel Okwi.
Simba walionekana kucheza vizuri hasa kipindi cha kwanza ingawa, walitengeneza nafasi chache za kufunga. Kurejea kwa kipa mzoefu, Ivo Mapunda baada ya kuwa nje ya dimba kutokana na majeruhi, kumeongezea nguvu kwenye kikosi cha kocha raia wa Zambia, Patrick Phiri.
Ruvu Shooting wameonyesha uimara hasa kwenye safu yao ya ulinzi licha ya kuwa wameruhusu bao hilo na kupoteza alama zote tatu. Ruvu Shooting wanaonyesha walikuwa wamejiandaa vema kuelekea mchezo wa leo hasa ukizingatia kuwa, wiki iliyopita walitoka kuchapwa na timu ya Coastal Union kule mkoani Tanga.
Elias Maguli ambaye aliingia kuchukuwa nafasi ya Said Ndemla, amechangia kwa kiasi kikubwa Simba kuibuka na ushindi kwani ni shuti lake ambalo lilimshinda kipa wa Ruvu Shooting Abdallah Rashid, ndipo Okwi alipopata nafasi ya kufunga bao la pekee na la tatu kwa msimu huu.
Kwaupande wa pili, timu ya Ndanda kutoka mkoa wa Mtwara imejikuta ikichezea kichapo kutoka kwa maafande wa JKT Ruvu cha mabao 2-0 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kipigo hicho kinatia doa sherehe zao ambazo zilikuwa zimeibuka baada ya wiki iliyopipa kuifunga Azam Fc bao 1-0 kule Nangwanda Sijaona huku ukiwa ndiyo mchezo wao wa kwanza kucheza chini ya kocha wao mpya, Abdul Mingange.
Matokeo ya mzunguko wa Saba wiki hii.
Yanga 2-0 Mgambo JKT
Mtibwa Sugar 1-1 Kagera Sugar
Polis Moro 1-0 Tanzania Prisons
Stand United 1-0 Mbeya City
Azam fc 2-1 Coastal Union
Ruvu JKT 2-0 Ndanda Fc
Simba 1-0 Ruvu Shooting
9 November 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment