Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 March 2014
Sunday, March 30, 2014

XAIV AMEMTAJA KOKE KAMA MBADALA WAKE.



Kiungo muhimu wa Uhispania na Barcelona Xavi amesema kiungo wa kati wa Atletico Madrid Koke anaweza kuwa mrithi wake kama kitovu cha mchezo wa kudhibiti mpira wa mabingwa hao wa dunia na Ulaya. 

Xavi, 34, anahitimisha uchezaji wake wa ufanisi mkubwa akichezea klabu na nchi na Koke mwenye miaka 22 ameibuka kuwa mmoja wa viungo wa kati wenye vipaji zaidi Uhispania pamoja na wengine kama vile Thiago Alcantara wa Bayern Munich na Isco wa Real Madrid. 

Xavi, ambaye amechukuliwa na wengi kama bora zaidi kwenye nafasi yake ya kudhibiti mpira kati, huenda atatangaza kustaafu kwake kwenye soka la kimataifa baada ya fainali za Kombe la Dunia nchni Brazil na anaamini kwamba Koke ana uwezo wa kuvaa viatu vyake. 

"Koke ni mchezaji wa kipekee,” Xavi alisema kwenye mahojiano yaliyochapishwa kwenye tovuti ya Atletico (www.clubatleticodemadrid.com) Jumapili kabla ya mechi ya kwanza ya robofainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya mahasimu hao wa La Liga Jumanne. 

"Ana kila kitu: kipaji, uwezo wa kimwili, yeye ni mwanasoka wa leo na siku za usoni,” Xavi aliongeza.
“Amegunduliwa kama mwelekezo wa bendi ya Uhispania kwa miaka 10 ijayo. 

“Ninampenda sana binafsi kwa sababu huwa tunacheza nafasi sawa na nafikiri ni mchezaji wa kipekee.”
Wote wawili, Xavi na Koke, huenda wakawepo kwenye kikosi cha Kombe la Dunia cha wachezaji 23 watakaoteuliwa na Vicente del Bosque. 

Uhispania watacheza mechi yao ya ufunguzi Kundi B dhidi ya Uholanzi mjini Salvador Juni 13, ambayo itakuwa marudio ya fainali ya 2010 ambayo Uhispania walishinda 1-0.
Watakutana na Chile mjini Rio De Janeiro Juni 18 na Australia mjini Curitiba siku tano baadaye.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!