Mshambuliaji Emmanuel Adebayor anaweza akawa njiani kuondoka White Hart Lane.
Tottenham Hotspur jana usiku ilikamilisha usajili wa kiungo wa kibrazil Paulinho kutoka Corinthians.Na sasa Andre Villas-Boas anahamishia akili yake katika ushambuliaji, huku mshambuliaji wa Valencia Roberto Soldado akiwa ndio chaguo lake la kwanza.
Boss huyo wa Spurs anategemea kumuuza Adebayor kwa klabu ya Besiktas ambayo ipo tayari kulipa kiasi cha £5m kwa ajili ya Mtogo huyo.
Dili hilo linaweza likamvutia zaidi Adebayor kutokana na kodi ndogo ya asilimia 15 wanayokatatwa wachezaji kwenye mishahara yao.
Adebayor, 29, ana mkataba wa miaka miwili na Spurs ambao unampatia kiasi cha £80,000 kwa wiki lakini anaonekana yupo njiani kuondoka.
Villas-Boas anataka kumuondoa mshambuliaji huyo wa Togo kwenye listi ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa ili amuongezea Soldado.
Tottenham wapo tayari kulipa kiasi cha £15m — lakini Valencia wanataka kiasi cha £25m.
Raisi wa Valencia Amadeo Salvo Lillo alisema: “Tumekuwa na matatizo mengi ya kifedha lakini hatuna ulazima wa kuanza kuuza wachezaji kwa bei zisizostahili”
Soldado, 28, alifunga mabao 30 katika mechi 46 alizocheza msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment