Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 November 2014
Saturday, November 29, 2014

David Moyes ang'ara ligi kuu Hispania.


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye kocha wa klabu ya Real Sociaded, David Moyes ameanza kung'ara kwenye ligi kuu nchini Hispania baada ya hapo jana kujipatia ushindi wa mabao 3-0 mbele ya timu ya Elche. 

Hii ilikuwa ni mechi ya pili kwa kocha huyo ambaye msimu uliopita alikuwa Meneja wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza.

Moyes alianza kibarua chake kwa kutoka sare na timu ya Deportivo la Coruna na hapo jana, alifanikiwa kuandikisha ushindi wake wa kwanza ingawa mchezo huo ulishuhudiwa na watazamaji wachache. 

Real Sociaded ilijipatia mabao yote kutoka kwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela ambaye alifunga Hat Trick katika mchezo huo.

Real Sociaded ambao walikuwa wanakamata nafasi ya 16 kwenye ligi, wameweza kupanda hadi nafasi ya 12 baada ya ushindi wa jana. Msimu huu Sociedad wameonekana kufanya vizuri hasa wanapocheza na vigogo lakini, wanapata tabu dhidi ya timu ndogo. 

Tayari wamefanikiwa kuwafunga msimu huu Atletico Madrid ambao ndiyo bingwa mtetezi na wababe wa Ulaya, Real Madrid. Katika mechi 10 za hivi karibuni dhidi ya timu za kati, Sociedad wamepata ushindi mara moja tu hivyo, ushindi dhidi ya Elche ni matokeo mazuri sana kwao.

Meneja huyo ambaye aliyedumu kwa miezi 10 tu na klabu ya Manchester United, anaonekana kuwa na mwanzo mzuri nchini Hispania baada ya kuboronga akiwa na miamba wa soka nchini Uingereza. Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Moyes kucheza akiwa uwanja wa nyumbani.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!