Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 October 2014
Wednesday, October 29, 2014

Yanga kuelekea Kaitaba


Na Oscar Oscar Jr

Timu ya wananchi, Dar es Salaam Young Africans inatarajia siku ya leo kushuka dimbani kumenyana na timu ya Ambassador ya mjni Kahama, katika mchezo wa kirafiki wakati timu hiyo ikijiandaa kuelekea mchezo wake na Kagera Sugar utakaochezwa kwenye dimba la Kaitaba mwishoni mwa juma hili.

Yanga wameweka kambi yao kwenye mji wa Kahama baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza kwenye mechi za kanda ya ziwa dhidi ya Stand United wiki iliyopita kwa mabao 3-0.

Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, akifunga mabao mawili ya mchezo huo mara baada ya kuingia akitokeo benchi na lingine, kufungwa na Mbrazil Jaja likiwa goli lake la kwanza la ligi kuu.

Yanga mpaka sasa, wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu na hii ni kutokana na kushuka dimbani mara tano huku wakiwa na alama sawa na Azam waliopo nafasi ya pili. 

Yanga walipoteza mechi yao ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar kabla ya hapo baadaye kushinda michezo mitatu na kutoka sare na mahasimu wao, timu ya Simba.

Kagera Sugar walianza ratiba yao ugenini kwa mechi tatu mfululizo na kujikusanyia alama tano kabla ya kurudi uwanja wa nyumbani na kutoka sare na Stand United na kutimiza alama sita. 

Kagera Sugar wako kwenye nafasi ya saba ya msimamo wa ligi kuu na watakuwa na kibarua kikubwa cha kupata alama tatu wakiwa nyumbani mbele ya Yanga.

Uwanja wa Kaitaba ni mahali pagumu sana kwa timu za wageni na msimu uliopita ni, timu tatu pekee ambazo zilifanikiwa kuondoka na ushindi katika dimba hilo na Yanga wakiwemo. 

Msimu huu umekuwa na mabadiliko makubwa kwa sababu, timu nyingi zinaonekana kufanya vizuri ugenini kuliko zinapocheza nyumbani.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!