Na Oscar Oscar Jr
Kiungo wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Arsenal, Jack Wilshere ameibuka na kuahidi magoli mengi kutoka kwake. Wilshere ni moja kati ya vijana wenye vipaji ingawa tatizo la majeruhi limekuwa likimrudisha nyuma kila msimu.
Mara kadhaa amekuwa akiwataja kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard na kiuno wa Manchester City, Frank Lampard kama role models wake.
Wilshere akizungumza kwenye mtandao wa timu ya Arsenal amesema, anapenda namna wachezaji hao wa kimataifa wa Uingereza enzi zao waliokuwa na uwezo wa kufunga magoli 15 hadi 20 kwa kila msimu.
Jack ambaye kiwango chake sasa kinaonekana kuimarika, atahakikisha anafunga magoli mengi ili kuisaidia timu yake.
Kiungo Aaron Ramsey alionyesha uwezo mkubwa sana msimu uliopita huku akifunga magoli 16 na kupiga pasi zilizopelekea kufungwa magoli tisa.
Ramsey alitangazwa mchezaji bora wa klabu msimu uliopita na kwa namna Jack Wilshere anavyozungumza ni kama anataka kufika kwenye kiwango hicho.
Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya tano baada ya kushuka dimbani mara tisa na kujikusanyia alama 14 huku Chelsea chini ya kocha Jose Mourinho wakiongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia alama 23 huku ikiwa ni timu pekee ambayo haijapoteza hata mchezo mmoja msimu huu.
0 comments:
Post a Comment