Na Chikoti Cico
Baada ya kuwa na matokeo mabovu dhidi ya Real Madrid kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya timu ya Liverpool inarejea tena uwanjani dhidi ya Hull City katika moja ya mechi za ligi kuu ya Uingereza itakayopigwa kwenye uwanja wa Anfield.
Liverpool wanaoshika nafasi ya sita wakiwa na alama 13 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kutafuta alama tatu muhimu nyumbani matokeo yanayoweza kuwapeleka mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ataendelea kumkosa mshambuliaji Mwingereza Daniel Strurridge ambaye bado ni majeruhi hivyo Mario Balotelli ambaye mpaka sasa ana goli moja kati ya mechi 10 aliyoichezea Liverpool anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Liverpool.
Takwimu zinaonyesha Liverpool imefunga magoli 10 katika mechi tatu za ligi walizocheza na Hull City kwenye uwanja wa Anfield huku nahodha Steven Gerrard akiwa na rekodi ya kufunga magoli matatu katika mechi mbili alizocheza dhidi ya Hull City nyumbani Anfield.
Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno; Gerrard, Henderson; Lallana, Coutinho, Sterling; Balotelli
Timu ya Hull City inatarajiwa kuwakosa mshambuliaji Nikica Jelavic na mabeki Michael Dawson na Andy Robertson huku makipa Allan McGergor na Steve Harper ambao ni chaguo la kwanza na la pili, nao pia watakosekana kwenye mchezo huo hali inayopolekea kwa kipa chaguo la tatu Eldin Jakupovic kuanza golini.
Timu ya Hully City inayofundishwa na kocha Steve Bruce mpaka sasa inashika nafasi ya 11 ikiwa na alama 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakitofautiana kwa alama tatu na Liverpool.
Takwimu zinaonyesha kati ya michezo 18 ya mashindano mbalimbali ambayo Hull City imecheza na Liverpool imeweza kushinda mchezo mmoja tu huku ikifungwa michezo 13 na kutoka sare michezo minne.
Kikosi cha Hull City kinaweza kuwa hivi: Jakupovic; Bruce, Chester, Davies; Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Diame, Robertson; Hernandez
0 comments:
Post a Comment