Liverpool vs Hull City
Na Rossa Kabwine
Brendan Rogers anataka timu yake ya Liverpool ifanye vizuri katika rekodi zake za ulinzi kuanzia mechi ya jumamosi dhidi ya hull city katika uwanja wa Anfield. Safu ya ulinzi ya Liverpool msimu uliopita, ilifungwa jumla ya magoli 50 katiaka mechi 38 wakati wakishika nafasi ya pili nyuma ya Manchester city.
Lakini Suarez na Daniel sturridge waliifungia timu hiyo jumla ya magoli 52. Walichangia zaidi ya nusu ya jumla ya magoli ya klabu hiyo, huku Suarez amabaye anachezea Barcelona kwasasa na Sturridge ambaye hajacheza tangu mwezi Agost kutokana na majeruhi, Rodgers anataka wajisikie fahari kwa kutoruhuhusu kufungwa (clean sheet).
Liverpool wameruhusu kufungwa magoli 12 katika michezo nane mpaka sasa na ni mchezo mmoja u dhidi ya Tottenham Hotspurs ambayo walishinda 3-0. Rogers akizungumzia kipigo cha 3-0 kutoka kwa Real Madrid, amesema “ Tunahitaji kufanya vizuri kama timu , sio kwa walinzi tu na golikipa pia”
Rogers aliongeza “ Magoli tuliofungwa mengi ni mepesi sana kwa hiyo, kazi yetu ni kufanya vizuri dhidi ya rekodi hiyo , hicho ndio kitu tunachokifanyia kazi. Wageni wa Liverpool wikendi hii watakuwa Hull city ambao wiki iliopita walitoka sare ya 2-1dhidi ya arsenal na Rodgers amekuwa akipendezwa na kazi alioifanya mpinzani wake, kocha Steve Bruce katika dirisha la usajiri. Je jitihada za Liverpool kutoruhusu goli zitafanikiwa leo dhidi ya Hull city?
0 comments:
Post a Comment