Na Chikoti Cico
Ligi kuu nchini Uingereza inatarajiwa kuendelea tena wikendi hii huku moja ya mechi zitakazopigwa siku ya Jumamosi ni kati ya Arsenal dhidi ya Burnley mchezo utakaopigwa saa 12 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa Emirates Stadium.
Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ataingia kwenye mchezo huo huku akiendelea kuwakosa Laurent Koscielny, Mesut Ozil, David Ospina , Yaya Sanogo, Abou Diaby, Olivier Giroud na Mathieu Debuchy ambao wote ni majeruhi.
Kiungo Jack Wilshere akiwa na hati hati ya kucheza mchezo huo kutokana na maumivu ya goti wakati huo huo, kocha Wenger amesema hataharakisha kumrejesha uwanjani winga Theo Walcott.
Timu ya Arsenal inayoshika nafasi ya tano ikiwa na alama 14 kati ya michezo tisa ya ligi inatarajiwa kuingia kwenye mchezo huo kutafuta alama tatu muhimu ili kupunguza “gap” la alama tisa kati yake na vinara Chelsea lakini pia, kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa kati ya timu nne za juu (top four) kwenye msimamo wa ligi.
Takwimu zinaonyesha katika michezo 22 iliyopita ya ligi kuu dhidi ya Burnely, timu ya Arsenal haijapoteza hata mchezo mmoja huku ikishinda michezo 14 na kutoka sare michezo nane, wakati huo huo katika michezo 10 iliyopita nyavu za Arsenal hazijatikiswa mara mbili tu.
Kikosi cha Arsenal kinaweza kuwa hivi: Szczesny; Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs; Arteta, Wilshere, Ramsey; Cazorla, Sanchez, Welbeck
Timu ya Burnley inayofundishwa na kocha Sean Dyche, inakabiliwa na wakati mgumu kwani mpaka sasa inashika mkia kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa na alama nne kati ya michezo tisa iliyocheza.
Katika mchezo huo dhidi ya Arsenal, kocha Dyche anatarajiwa kuwakosa Sam Vokes, Matt Taylor na Stephen Reid ambao bado wanauuguza majeraha huku Dean Marney, akitarajiwa kurejea uwanjani bada ya kuwa nje kwa muda.
Takwimu zinaonyesha mpaka sasa timu ya Burnley imefungwa jumla ya magoli 12 katika michezo minne iliyopita ya ligi huku mpaka sasa, hawajashinda mchezo wowote ule kati ya michezo tisa iliyocheza.
hivyo, jopo la makocha wa Burnleny wana kazi kubwa ya kupigana kufa na kupona ili kuondoka mkiani.
Kikosi cha Burnley kinaweza kuwa hivi: Heaton; Tripper, Shackell, Duff, Ward; Kightly, Jones, Chalobah, Arfield; Boyd, Ings
0 comments:
Post a Comment