Azam wamefika zao Mtwara kuisambaratisha Ndanda fc
Na Oscar Oscar Jr
Bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzani bara, timu ya Azam wame elekea mkoani Mtwara kwa ajiri ya kujiandaa na mchezo wao weekend hii dhidi ya timu inayosua sua ya Ndanda fc.
Ndanda wako kwenye nafasi ya 13 baada ya kushuka dimbani mara tano na kushinda mchezo mmoja pekee huku wakichezea kichapo mara nne.
Azam ambao wameweka rekodi ya kucheza michezo 38 ya ligi kuu bila kupoteza, weekend iliyopita walijikuta wakichezea kichapo kwenye uwanja wa nyumbani, Azam Complex toka kwa maafande wa JKT Ruvu chini ya kocha mzawa Felix Minziro.
Azam wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi huku wakiwa na pointi 10 sawa na timu ya Wananchi, Dar es salaam Young Africans wanaoshika nafasi ya tatu baada ya wote kushuka dimbani mara tano na kila mmoja, akichezea kichapo mara moja.
Majeruhi wa Azam wa muda mrefu ni Naahodha John Boccco, Lionel Saint Preux, Ismail Diara na Frank Domayo ambaye hajacheza hata mechi moja ya ligi tangu ajiunge na mabingwa hao akitokea timu ya Yanga.
Lionel Saint Preux tayari ameanza mazoezi na amesafiri na timu mkoani Mtwara huku, hao wengine tarehe ya kurudi uwanjani ikiwa haijulikani.
Didier Kavumbagu ambaye alianza kwa kasi upachikaji wa magoli akiwa na magoli manne, anaonekana kusua sua baada ya mechi mbili zilizopita kushindwa kupachika hata goli moja.
presha itaanza kuongezeke kwake hasa baada ya Ally Shomary na Ame Ally wa Mtibwa Sugar, kumkaribia kwa magoli kwani hao wote wamefikisha magoli matatu kila mmoja, huku Kavumbagu akibakia na magoli yake yale yale.
0 comments:
Post a Comment