Michael Carrick yuko njiani kurudi.
Na Ezekiel Kavenga
Angel Di maria na kiungo Ander Herrera, wapo fiti katika pambano la kesho dhidi ya Chelsea. Wachezaji hao wamefaulu vipimo vya afya kuelekea mchezo wa Jumapili.
Viungo hao wote walikua katika hali ya mashaka baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya 2-2 wa Jumatatu dhidi ya West Bromwich Albion.
Lakini Manager Louis Van Gaal amethibitisha uwepo wa wachezaji hao wawili Japokuwa kiungo mwingine Michael Carrick, ataendelea kujiimarisha zaidi kwa kuchezea timu ya wachezaji wa akiba akianzia jana kwenye pambano dhidi ya wachezaji wa akiba wa West ham United.
kocha Loius Van gaal alisema "Herrera yupo teyari kwa mchezo unaofuata pamoja na Di maria, Carrick atakuwa nje bado anatafuta uimara katika mchezo na Rooney anatumikia adhabu"
0 comments:
Post a Comment