Manuel Pellegrini asema mambo bado
Na Rossa Kabwine
Meneja wa Manchester city, Maunel pellegrin amekataa kukiri kama kipigo chao cha jana kinaweza kuwa tatizo kueleke mbio za ubingwa ambapo Chelsea mpaka sasa, wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 22.
Chelsea wanaweza kuongeza pengo hilo kama watapata ushindi au draw dhidi ya Manchester united mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu majira ya saa 1:00 leo jumapili.
“Ndiyo tumeanza ligi na bado tuna pointi 87 zimebaki za kugombea. So ni mapema “ alisema pellegrin. Kocha huyo rai wa Chile aliongeza “tutaendelea kupambana kwa kuwa hakuna taji ambalo lime kabidhiwa kwa sasa kwa timu yoyo"
Kufungwa kwa city imehitimisha wiki ya machungu kwa mabingwa hao wa uingereza, baada ya kutoka sare ya 2-2 dhidi ya CSKA Moscow katikati ya wiki na Kushindwa katika uwanja wa Upton Park ya West Ham United ina maanisha Manchester City wameshuka kwa pointi 10 kutoka kwenye michezo yake tisa ya ufunguzi.
Pellegrini alisisitiza kuwa, msimu uliopita timu yake ilikuwa katika hatua hiyohiyo baada ya michezo tisa, baada ya kufungwa na Chelsea, City walikuwa kwenye nafasi ya saba.
Pellegrini alisisitiza kuwa anaendelea kuwaamini wachezaji wake ingawa alikili anatambua kuwa kitendo cha timu yake kutofanya vizuri kipindi cha kwanza dhidi ya West Ham, kuliwagharimu.
Kazi ya Morgan Amalfitano na Diafra Sakho jana ziliwafanya wawe mbele kwa goili 2-0 ingawa baadae david silva kufunga goli moja na baada ya dakika 90 kumalizika, Manchester City walikubali kichapo cha mara ya pili msimu huu.
0 comments:
Post a Comment