Mesut Ozil kutimka Arsenal?
Na Rossa Kabwine
Meneja wa Manchester city Manuel Pelllegrini ameripotiwa kuiamrisha klabu yake ya machester city kumsajili mchezaji wa Arsenal, Mesut Ozil katika dirisha la Januari kama mbadala wa Yaya Toure
City imekuwa ikuhusishwa na uhamisho wa Ozil wa paundi milioni 32 kwa siku chache zilizopita na washika bunduki, timu ya Arsenal wameripotiwa kuwa tayari kupokea pesa hizo kwa kwa ajili ya mchezaji huyo wakimataifa wa Ujerumani.
Kwa sasa ripoti zinasema meneja wa City, Pellegrini ndiye aliyeomba klabu yake imsajili Ozil wakati wa dirisha dogo huku nyota wa Ivory coast, Yaya Toure akionekana kuondoka klabuni hapo.
PSG na Monaco wote wamekuwa wakihusishwa kwa uhamisho mkubwa wa Toure na City wanataka kumpata Ozil ili kuziba nafasi ya toure ya mchango wake katika ushambuliaji.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.