Majanga ya washambuliaji Chelsea
Na Rossa Kabwine
Kuelekea mchezo kati ya Manchester united na Chelsea Mshambuliaji wa Chelsea Loic Remy, kuna matumaini kuwa atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Manchester United ingawa ana sumbuliwa na maumivu ya nyonga.
Remy aliumia katika mchezo dhidi ya Maribor siku ya jumanne na kocha Jose Mourinho amekuwa na mataraijio ya kwenda Old Trafford jumapili hii bila kuwa na washambuliaji wake wakutegemewa.
Didier Drogba ambaye ametoka kuuguza kifundo cha mguu anatarajia kuongoza safu ya ushambuliaji katika mechi hiyo. Diego Costa amekosa mechi mbili akikabiliwa na maumivu ya misuli na Remy alitolewa dakiaka ya 16 ya mchezo kati ya Chelsea na Maribor ambapo Chelsea ili iadhibu viakali Maribor kwa kuifunga magoli 6-0.
Remy alisema “nyonga ilikaza kidogo na sikujisikia vizuri ndio maana nlipenda nitoke , kama sijisikii vizuri sana ni vyema nitoke na kumpisha mchezaji alie fiti kwa asilimia mia moja"
Remy aliongeza kuwa “ ntaangalia vipimo naamini sio tatizo kubwa. Uzuri sikuendelea kucheza kwa sababu kuna kitu nlikuwa najisikia sijui kama kilikuwa kibaya sana lakini kuna kitu nlijisikia”
Chelsea itakuna na man united old Trafford katika mchezo wa ligi kuu ya uiengereza tarehe 26/10/2014 ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa kujikusanyia alama 22 kwenye mechezo nane.
0 comments:
Post a Comment