Mzimu wa sare unaoitesa Simba, wamalizika Iringa.
Na Oscar Oscar Jr
Timu ya Simba imeweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli fc ya Mkoani Iringa mchezo ulipigwa kwenye dimba la Samora na kupachikwa wavuni na mshambuliaji Elius Maguli.
Maguli ameonekana kuaminiwa na kocha Mzambia Patrick Phiri kutokana na uwezo mkubwa anaoonyesha dimbani.
Simba wako mkoani Iringa wakijiandaa na mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar ya morogoro itakayopigwa Jumamosi hii kwenye dimba la Jamhuri.
Elias Maguli ambaye alifunga mabao 13 msimu uliopita, ameonekana kumvutia kocha wake ambaye anaonekana kumkubali zaidi kuliko mfungaji bora wa msimu uliopita, Mrundi Amis Tambwe.
Ushindi huo unaweza kuongeza morali ya wachezaji na benchi la ufundi ambao wako kwenye presha ya juu kutoka kwa viongozi na wanachama wa timu hiyo kufuatia matokeo ya sare kwenye michezo mitano ya ligi kuu.
Benchi la ufundi la klabu hiyo, limepewa mechi mbili tu za kuthibitisha uwezo wao na endapo matokeo hayatokuwa mazuri ni wazi kuwa kuna watendaji watafukuzwa kazi.
0 comments:
Post a Comment