Huu ndiyo Mtihani mkubwa wa kocha Maximo kwa sasa.
Na Samuel Samuel
Mechi ya jumamosi kati ya Dar Young African na wana Nkurukumbi, Kagera Sugar kuna mitihani mizito miwili kwa Maximo .
Yanga inayokwenda kuwavaa Kagera ina kumbu kumbu nzuri ya ushindi wa jumamosi dhidi ya Stand United. Yanga iliwabamiza 3-0 Stand huku mchezaji kipenzi wa klabu hiyo, Tegete akitupia kwenye kamba magoli mawili.
Mtihani wa kwanza wa Maximo, ni shinikizo la meneja wa kipa namba mbili wa klabu hiyo Juma Kaseja. Kwa nyakati tofauti amekaririwa akisema halidhishwi na matumizi ya mchezaji huyo ndani ya kikosi hicho .
Kaseja amekuwa hana uhakika wa kucheza ndani ya klabu hiyo na kumuacha Dida akizidi kung'ara. Meneja huyo ameonya kama mchezaji huyo hatapangwa katika mechi nane zilizobaki, basi atamuondoa mteja wake hapo jangwani.
Je hali hiyo itamfanya Maximo ampange kikosi cha kwanza mkongwe huyo ? Baada ya mechi hiyo Yanga itacheza na Mgambo jijini Dar palipo na mashabiki lukuki wa klabu hiyo wasio na imani na kipa huyo.
Hivyo sidhani Maximo kama anaweza kumpanga mchezaji huyo jijini maana atakuwa chini ya pressure kubwa. Hivyo Maximo yupo katika mtihani mzito.
Mtihani wa pili , ni mashabiki wa Yanga wanataka kuona je ataendelea kumtumia Tegete au atarudi benchi? Maamuzi ya mwisho anayo kocha.
0 comments:
Post a Comment