Na Chikoti Cico
Baada
ya mechi kati ya Manchester United na Chelsa kuisha kwa sare ya
kufungana kwa goli 1-1, mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford
kocha wa Chelsea Jose Mourinho, akwepa kumzungumzia refa wa mchezo huo
Phil Dowd wakati akihojiwa na waandishi wa habari.
Chelsea walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye dakika ya 53 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Didier Drogba aliyeunganisha kona iliyochongwa na Fabregas kabla ya Manchester United kusawazisha goli hilo kwenye dakika ya 94 ya mchezo kupitia kwa Robin Van Persie.
Kocha Jose Mourinho akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo huo alisema “ Kwasasa tuna nafasi ndogo kwa makosa yetu ama kwa makosa ya waamuzi, kama nikisema kilichoko moyoni mwangu ntakuwa matatizoni nimechagua kutokuzungumzia kitendo hiki (Ivanovic kupewa kadi nyekundu), kulikuwa na mambo mengi yaliyoenda kinyume na sisi matokeo hayakuwa mazuri sana lakini yanakubalika”.
Kwa matokeo hayo Chelsea bado wanaongoza kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kwa tofauti ya alama nne dhidi ya Southampton walioko nafasi ya pili wakiwa na alama 19 huku Manchester United wakiwa nafasi ya nane wakiwa na alama 13.
Mourinho akiendelea kuongea na waandishi wa habari aliisifu timu yake kwa kusema “ Nina furaha kwa timu yangu walicheza mchezo mzuri, sio rahisi kucheza dhidi ya Manchester United timu inayocheza kwa kusogeleana na kwa mipira ya kushitukiza aliendelea kusema “tungeweza kufunga magoli mengi zaidi hasa lile la Hazard ingawa ninajivunia wachezaji wang.
Kocha Mourinho hakusita kumsifia mshambuliaji wake Didier Drogba kwa jinsi alivyocheza mchezo huo kwa kusema “ Hakuweza hata kufanya mazoezi na kucheza kwa dakika 90 kama leo (jana), hivyo nina furaha kwa jinsi alivyocheza. Drogba amefunga magoli mengi kama hili”

0 comments:
Post a Comment