Angel Di Maria kuwavaa Chelsea Old Trafford
Na Rossa Kabwine
Meneja wa Manchester united, Loius Van Gaal amethibitisha winga Angel di Maria amefanya mazoezi wiki hii na atakuwa fiti kukutana na Chelsea jumapili hii.
Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Argentina, aliumia jumatatu wiki hii katika mchezo dhidi ya Westbromwich Albion amabao ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya 2-2 ulio mfanya kuwa na wasiwasi kwa mechi ya jumapili dhidi ya Chelsea .
Lakin Van Gaal amedhihirisha katika mahojiano siku ya ijumaa kuwa, mchezaji huyo anayeshikilia rekodi ya uhamisho klabuni hapo, amefanya mazoezi tangu alhamis katika maandalizi ya mechi hiyo itakayopigwa mwishoni mwa juma hili.
Hakuna mchezaji mwingine ambaye amerudi kutoka majeruhi katika timu hiyo , lakini Carrick atacheza na wachezaji wa akiba dhidi ya timu yake ya zamani ya West Ham United baada ya kukaa nje kwa muda wa miezi mitano.
0 comments:
Post a Comment