Kitakacho isumbua simba kwenye mechi na mtibwa.
Na Samuel Samuel
Simba SC inakwenda kupambana na vinara wa ligi kuu Tanzania bara, timu ya Mtibwa Sukari katika mazingira ya kutia hofu sana. Kinachoendelea ndani ya klabu hiyo kongwe nchini ni hali ya kusikitisha sana.
Klabu hiyo yenye masikani mtaa wa Msimbazi, kariakoo Dar es Salaam mpaka sasa imecheza michezo mitano na kujikusanyia pointi tano kutokana na kutoka sare michezo yote.
Mtibwa Sugar inayomtegemea sana kiungo wake mshambuliaji, Mzamilu ambaye mechi ya ufunguzi aliwasumbua sana mabeki wa Yanga, wanaikaribisha Simba wakiwa na morali ya juu kwa mambo yafuatayo;
Kwanza kabisa wapo vizuri kisaikolojia kutokana na ushidi waliopata kwenye mechi nne na kudroo mechi moja. Hali hiyo inawajengea hali ya kujiamini na hamasa ya kutaka kushinda zaidi.
Pili timu yeyote ile mbali na Simba na Yanga inapofanikiwa kuifunga moja timu hizo, huamini inaweza kuifunga na nyenzake. Mtibwa ina kumbu kumbu ya kuifunga Yanga hivyo wana imani jumamosi wataweza kuiangusha pia miamba hiyo.
Tatu, Mtibwa Sugar wanaweza kuitumia fursa ya sitofahamu inayoendelea kwenye klabu hiyo na kujipatia ushindi. Benchi la ufundi la Simba ambalo lipo chini ya kocha mkuu Patrick Phiri na msaidizi wake Suleimani Matola, wamepewa mechi mbili kushinda wakianzia na mechi hiyo.
Kitendo kinawaweka waalimu hao chini ya msongo mkubwa hivyo ufanisi utapungua. Kusimamishwa kwa baadhi ya wachezaji wa Simba kwa tuhuma za kucheza chini ya kiwango.
Hali hiyo inaweza kuwafanya wachezaji waliobaki kucheza kwa tension kubwa kuogopa lawama na mwisho wa siku wakaua muunganiko wa timu na kuwapa wachezaji mahili wa Mtibwa kama kuichachafya timu hiyo.
Lakini kiufundi Mtibwa wasitegemee mteremko bado wekundu hao wa msimbazi wana nafasi ya kuondoka na pointi tatu. Mtibwa wanatumia 4-5-1 Mara nyingi wanapocheza na timu hizi mbili lakini Phiri ambaye mchezo uliopita na Prisons alitumia 4-3-1-2 mfumo ambao alikusudia kupata magoli mengi.
Mchezo utakuwa mgumu kwa fomesheni hizo hasa baada ya daktari wa Simba kuthibitisha kiungo mkabaji wa timu hiyo Mkude atacheza mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment