Coutinho asaini mkataba mpya Liverpool
Na Florence George
Kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho amekubali kuongeza mkataba wa muda mrefu wa kuichezea timu hiyo ambaye mkataba wake wa sasa ulikuwa unamalizika mwaka 2018 hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Liverpool iliyotolewa siku ya Jumanne.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ameshaichezea Liverpool michezo 81 tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Inter Milan ya nchini Italia mwaka 2013 na amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi hicho cha Brendan Rodgers .
Kwa mujibu wa vyombo vya Habari mkataba huyo utamuweka Coutinho katika timu hiyo hadi mwaka 2020.
Coutinho aliuambia mtandao wa Liverpool kuwa "timu hii iliniamini na kunipa nafasi kubwa ya kucheza japo kuwa nilikuwa sichezi mara kwa mara katika timu yangu ya awali".
Alimalizia kwa kusema kuwa "Liverpool ni familia kubwa na binafsi ninafuraha kuwa katika timu hii",mpaka sasa mchezaji huyo amefunga magoli mawili katika michezo 31 aliyoichezea timu hiyo katika michuano mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment