Jose Mourinho atuma ujumbe wa Pongezi.
Na Oscar Oscar Jr
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ametuma ujumbe wa pongezi kwa kocha mkuu wa timu ya West Ham United, Sam Allardyce kwa mwanzo mzuri wa msimu na hasa baada ya kuwafunga Manchester City weekend hii kwa mabao 2-1.
Sam Allardyce na Mourinho walitofautiana msimu uliopita kwenye mchezo uliozikutanisha timu zao pale katika dimba la Stanfford Bridge na kumalizika kwa Suluhu huku kocha wa Chelsea, akimshutumu mwenzie kwa kucheza mchezo ambao aliita wa karne ya 19.
West Ham United wameshinda michezo mitano mpaka sasa, wametoka sare mara tatu na kupoteza michezo mitatu pekee. Tofauti ya West Ham United wanaoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza na Manchester City wanaoshika nafasi ya tatu, ni pointi moja pekee.
0 comments:
Post a Comment