Na Chikoti Cico
Kuelekea kwenye mechi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya Liverpool dhidi ya Real Madrid itakayopigwa kwenye uwanja wa Anfied kiungo na nahodha wa timu ya liverpool Steven Gerrard antumai liverpool watarejea kwa kile walichokifanya mwaka 2009 baada ya kuifunga Real Madrid kwa magoli 4-0 na kuingia hatua ya robo fainali huku gerrard akifunga magoli mawili kwenye mechi hiyo.
Gerrard akiongea na waandishi alisema “Kila mmoja anaijua klabu hii na historia yake na ni muhimu ligi ya Mabingwa wa Ulaya kubaki hapa kadri tunavyoweza, usiku ule ulikuwa mzuri kwangu na timu ya 2009, ulikuwa mchezo bora wa timu na tunatarajia timu kucheza kama hivyo kesho (leo) usiku kama tunataka matokeo mazuri.
Gerrard aliyenyakua kombe la ligi ya mabingwa wa Ulaya na Liverpool mara ya mwisho mwaka 2005 dhidi ya AC Milan aliendelea kusema “ Nikiangalia nyuma kwenye mechi ile sababu iliyofanya tuwe juu ni kwasababu tulikuwa wapiganaji tulipokuwa na mpira na tulipokuwa hatuna, tulikaba kuanzia mbele lakini pia tulikuwa na kipaji bora cha dunia kutoka kwa Fernando Torres ambaye alicheza vyema na wote tulikuwa nyuma yake usiku huo”
Lakini pamoja na Gerrard kutaka Liverpool kufanya kama walivyofanya usiku ule wa 2009 dhidi ya Real Madrid bado Gerrard hakusita kukubali ubora wa Madrid kwasasa aliposema”Nikiwa na heshima kwa timu ya mwaka 2009, Real Madrid wameendelea na kuimarika kama walivyoonyesha mwaka jana ni timu bora hivyo tunaheshima kwa timu mpya ya Real Madrid”
Mwisho nahodha huyo wa Liverpool alimwongelea mshambuliaji wa Madrid Christiano Ronaldo akisema“ Kwasasa bila shaka ni mchezaji bora duniani, na ameimarika mwaka hadi mwaka na magoli anayofunga kwasasa anaweka rekodi ni mchezaji wa pekee, ni muhimu tusiende kwenye mechi hii tukihofu kuhusu Christiano itakuwa ni kuwakosea heshima wachezaji wengine wa Real Madrid”
Gerrard aliendelea kusema “Lengo langu ni kwa wachezaji wenzangu na wachezaji bora tulionao, ni muhimu tujaribu kucheza vyema kwa pamoja na tujaribu kufanya ugumu (kwa Madrid) tunavyoweza”
0 comments:
Post a Comment