Arsenal wanataka kuongeza nguvu January.
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 weekend iliyopita dhidi ya timu ya Sunderland, Arsenal wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 14 huku vinara timu ya Chelsea wakitoka sare ya 1-1 na Manchester United na kubakia kileleni.
Kocha wa Arsenal bado hajapa tiba ya kiungo mkabaji baaada ya Nahodha wake Mikel Arteta na mfaransa, Methieu Flamini kuonekana kushindwa nafasi hiyo.
Magazeti yameendelea kuripo uwepo wa kumnasa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani na Real Madrid, Semi Khedira kipindi cha dirisha dogo la usajili.
Khedira amekuwa akihusishwa na vijana hao wa London Kaskazini lakini, mshahara mkubwa anaohitaji kiungo huyo umekuwa kikwazo kwa kocha Arsene Wenger. Kuna habari kuwa Khedira ambaye mkataba na Real Madrid utamalizika mwishoni mwa msimu huu, amepunguza mshahara na kudai Pauni 80,000 kwa wiki.
Majeruhi ya beki wa kati Laurent Konscienley, yanapelekea beki rai wa Hispania Nacho Monreal kucheza kama mlinzi wa kati. Wenger ameripotiwa kumnyatia mchezaji wa Uholanzi na klabu ya Celtic, Virgil van Dijk.
Kwa upande wa pili, kiungo wa timu ya West Ham United, Winston Reid yuko njiani kujiunga na Gunners mwezi January. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Gazeti la The daily Mirror.
Kwa upande wa Daily Express, wao wameendelea kumtaja winga wa kimataifa wa Hispania na Barcelona Pedro Rodriguez, kutaka ujiunga na washika Bunduki hao mwezi January.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Pedro Rodriguez tayari amewasilisha ombi la kuondoka kwenye klabu hiyo kufuatia kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Luiz Enrique.
0 comments:
Post a Comment