Aston villa wana nafasi ya kumsajili kiungo wa Manchester united
Na Rossa Kabwine
Aston villa wana nafasi ya kumsajili kiungo wa Manchester united Tom Cleverly kwa uhamisho wa kudumu. Kiungo huyo wa amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo kataika dirisha la usajil la majira ya joto na tayari ameichezea timu yake mpya ya ston vila mechi tano katika ligi kuu ya uingereza na amemshawishi menejawake wa villa Paul Lambert.
Kocha huyo ametanabaisha kuwa, Aston villa wana nafasi ya kumsajili cleverly mwezi Januari. Lambert amethibitisha kuwa, mchezaji huyo mwenye miaka 25 ambaye mkataba wake na Manchester united unaisha msimu huu, anaweza kupata uhamisho wa kudumu aston villa mwezi januari.
“Tuna nafasi kwa Tom, hatujaingi kiundani zaidi lakini kacheza vizuri” Lambert alisema. Villa kwasasa wamefungwa mechi nne baada ya kuanza vizuri msimu huu. Lambert ambaye ataangalia afya za mabeki wa timu yake Phlippe Sendros na Nathan Baker, kama watakuwa sawa kuelekea mchezo wao wa Jumatatu dhidi ya timu ya QPR.
0 comments:
Post a Comment