Na Oscar Oscar Jr
Real Madrid jana walijikuta wakichezea kichapo cha mabao 4-2 toka kwa vijana wa Real Sociedad na kumfanya nahodha wa timu hiyo Iker Casillas kutoridhishwa na namna walivyocheza.
Real Madrid imejikuta ikitumia pesa nyingi kuleta wachezaji wa kawaida na kuruhusu wachezaji imara kutimka.
Tayari Real Madrid ilimruhusu Mesut Ozil kujiunga na Arsenal msimu uliopita huku Angel Di maria msimu huu akijiunga na Manchester United na Xaib Alonso akiondoka na kujiunga na mabingwa wa Bundesliga timu ya Bayern Munich.
Bado hali si shwari kwa watoto hao wa mfalme licha ya kuwaongeza kikosini Ton Kroos na James Rodriquez. Jana hawakuweza kuwa na mchezaji wao bora wa dunia na Ulaya kwa sasa, Christiano Ronaldo ambaye yuko nje kutokana na kuwa majeruhi.
Real Madrid kwa sasa wanamtengemea mshambuliaji mmoja tu Karim Benzema ingawa kuna taarifa za kumsajili Javier Hernandez kwa mkopo akitokea klabu ya Manchester United.
Safu ya ulinzi inayoundwa na Pepe na Sergio Ramos bado haionekani kutimiza majukumu yao ya msingi na pengine huu ni muda muafaka kwa kocha Carlo Ancelotti kuangalia uwezekano wa kumpa nafasi Raphael Varane.
Nahodha wa miamba Real Madrid, Iker Casillas, amekashifu mchezo wao duni baada ya kusalimisha uongozi wa 2-0 kulazwa 4-2 na Real Sociedad katika ligi ya Uhispania, La Liga, Jumapili.
Matokeo hayo ya mshtuko walizua maswali mengi wa uwezo wa kikosi hicho ghali zaidi duniani kujimudu bila huduma za mchezaji bora zaidi duniani, Cristiano Ronaldo, ambaye kwa mara nyingine tena, alikosa kucheza kutokana na jeraha.
Inigo Martinez na Carlos Vela walifunga goli moja kila mtu huku David Zurutuza, akifunga mabao mawili kwa upande wa Real Sociedad. Magoli ya mapema kutoka Sergio Ramos na Gareth Bale kwa upande wa Real Madrid hayakuweza kuwapatia ushindi katika mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment