Na Chicoti (Cico cicod)
0755 700 076
Katika umri wa miaka 32 mshambuliaji na Nahodha wa Sweden anayekipiga kwenye klabu ya PSG Zlatan Ibrahimovic aweka rekodi mpya ya magoli kwa timu ya taifa ya Sweden hii ni baada ya kufunga magoli mawili kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Estonia iliyoisha kwa Sweden kushinda kwa magoli 2-0.
Kwa kufunga magoli hayo mawili Ibrahimovic ameweza kufikisha jumla ya magoli 50 katika mechi 99 alizoichezea Sweden na kuweka rekodi mpya akiivunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Sven Rydell ya magoli 49 katika mechi 43 iliyowekwa mwaka 1932.
Katika kuonyesha furaha aliyonayo baada ya kufunga goli la pili kwenye mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Estonia Zlatan alivua jezi na kuonyesha maandishi kwa mashabiki yaliyosomeka “magoli 50, mmeyafanya yawezekane”.
Baada ya mechi dhidi ya Estonia Ibrahimovic akihojiwa na waandishi wa habari alisema “Kuvunja rekodi inamaana kubwa sana kwangu, ina umuhimu kwangu, kwa familia yangu na kwa watu wanaonizunguka” aliendelea kusema “wakati wote nimekuwa nikipigana kufanikisha malengo yangu bila kukata tama, jina langu sasa linaongoza kwenye orodha ya wafungaji wa Sweden na hiyo ni hisia nzuri”
0 comments:
Post a Comment