Arsenal kusajili mshambuliaji?
Na Oscar Oscar Jr
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ameendelea kumtetea mshambuliaji Yaya Sanogo ambaye katika mchezo wao dhidi ya Lecester City alipata nafasi nyingi za kufunga lakini hakufanya hivyo.
Wenger amesema Sanogo ni mchezaji mzuri na bado ana umri mdogo hivyo anajukumu la kuimarika zaidi na mashabiki ni lazima wawe wavumilivu.
Wakati mashabiki wa timu hiyo wakiendelea kuwa na shauku ya kupata mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kuongeza nguvu, kocha Arsene Wenger ameendelea kusisitiza kuwa, kununua wachezaji kwa sababu ya kutofanya vizuri kwenye mchezo mmoja sio njia ya kutatua tatizo.
Pamoja na kuwa timu ya arsenal inatatizo la kukosa kiungo mahiri wa kukaba na mshambuliaji wa kiwango cha juu, uteuzi wa kikosi na kuchelewa kufanya mabadiliko ya haraka kunakofanywa na kocha Arsene Wenger kunapelekea timu hiyo kushindwa kufanya vizuri.
Bado kocha huyo amegoma kumpa nafasi kiungo mshambuliaji Tomas Rosicky na mshambuliaji Lukas Podolski huku wachezaji wake wengi wanaonekana kuwa na uchovu.
Baada ya kutoka sare kwenye michezo yao miwili dhidi ya Everton na Lecester City huku ushindi pekee ukipatikana dhidi ya Crystal Palace, mechi ijayo watakutana na Manchester City.
0 comments:
Post a Comment