Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 August 2014
Sunday, August 31, 2014

Umeshamuelewa Mourinho?



 Na Oscar Oscar Jr

Wakati msimu uliopita kocha wa Chelsea alipokuwa analalamika tatizo la kukosa mshambuliaji, watu wengi hawakumuelewa. Wengi walichukulia kama analeta janja janja kwa sababu ukiwatazama Demba Ba, Fernando Torres na Samuel Eto'o walikuwa na sifa ya kuwapatia ubingwa.

Mourinho  ni kocha anayejiamini na anayeijua vema kazi yake. Tayari dunia inajua kwa sasa Diego Costa ni kiumbe wa aina gani na upande wa pili, watu wamepata fursa ya kuziona tena pasi za mwisho za Cesc Fabregas. Cesc ametoa pasi tano kwenye mechi tatu huku Costa akifunga mabao manne katika mechi tatu.

Chelsea jana walifunga mabao sita mbele ya Everton pale katika dimba la Goodison Park huku vijana wa kocha Roberto Martinez wakijibu mapigo kwa kufunga mabao matatu. 

Mabao ya mapema kutoka kwa Costa na Ivanovic yaliwapoteza mwelekeo Everton na kujikuta wakihaha dimbani.

Bado Chelsea ni timu imara na wana kikosi kipana chenye ubora, safari ya ligi kuu Uingereza ni ndefu lakini wanaonekana msimu huu kuwa hatari zaidi. 

Romelu Lukaku na Samuel Eto'o jana walikipiga kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yao ya zamani na Eto'o alifanikiwa kufunga bao moja.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!