Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 August 2014
Monday, August 25, 2014

Real Madrid dimbani leo usiku



 Na Oscar Oscar Jr

Real Madrid wana shinikizo kubwa la kutwaa taji la nyumbani na La Liga, musimu huu baada ya kukusanya kikosi ghali zaidi duniani.

Msimu uliopita walifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ulaya na Ule wa Mfalme na dakika za mwisho walijikuta wakipoteza nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi uliochukuliwa na mahasimu wao klabu ya Atletico Madrid.

Licha ya kutumia zaidi ya euro milioni 100 kuongezea nyota wa Kombe la Dunia James Rodriguez, Toni Kroos na Keylor Navas, Real walilazwa kwenye mechi ya marudiano na majirani zao, Atletico Madrid, kwenye kombe la Supa Copa na kupelekea kuzua hofu kuwa hawako tayari kuanza msimu huu vyema. 

Real wataanza kampeni yao dhidi ya Cordoba waliopanda daraja usiku wa leo na ikiwa kiungo Angel Di Maria ataondoka kama inavyo tarajiwa, kocha Carlo Ancelotti atakuwa na jukumu la kuteua mchezaji mwingine ili kuziba nafasi ya kiungo huyo raia wa Argentina.

Tayari, mjadala umezuka ni nani kati ya nahodha mkongwe, Iker Casillas na Navas anafaa kuanza langoni huku viungo wa hispania, Isco na Asier Illarramendi, waliogharimu euro milioni 70 kuwasajili mwaka jana wakitishiwa na kipindi kirefu pembeni mwa kikosi cha kwanza. 


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!